Mlango

← Rudi Mlango

Jinsi ya kufuta taarifa zako

Unaweza kutuomba tufute taarifa binafsi ambazo Mlango inazo kukuhusu wakati wowote. Hatua za kufuata zinategemea kama una akaunti ya Mlango, au ulipokea ujumbe wa WhatsApp kutoka kwa biashara inayotumia Mlango.

Imesasishwa: 6 Oktoba 2026

01Ikiwa ulipokea ujumbe wa WhatsApp kupitia Mlango

Kuacha kupokea ujumbe, jibu STOP au ACHA kwenye ujumbe wowote kutoka kwa biashara hiyo. Utaondolewa mara moja kwenye kampeni na vikumbusho vyake.

Kufutiwa taarifa zako:

  • Tuma barua pepe kwa habari@mlango.co.tz yenye kichwa Futa taarifa zangu.
  • Taja namba ya simu iliyopokea ujumbe na, kama unaweza, jina la biashara iliyokutumia.
  • Tutathibitisha — kwa kukujibu, au kwa ujumbe wa WhatsApp kwenda namba hiyo — kwamba ombi kweli linatoka kwa mmiliki wa namba hiyo.

Tunafuta namba yako, jina lako, ujumbe uliotumiwa na majibu yako kutoka kwenye akaunti za biashara zilizowasiliana nawe kupitia Mlango, na tunazijulisha biashara hizo kwamba tumefanya hivyo. Unaweza pia kuiomba biashara husika moja kwa moja — inaweza kukufuta kwenye akaunti yake ya Mlango.

02Ikiwa una akaunti ya Mlango

  • Tuma barua pepe kwa habari@mlango.co.tz kutoka kwenye barua pepe iliyosajiliwa kwenye akaunti yako, yenye kichwa Futa akaunti yangu ya Mlango.
  • Tueleze kama unataka salio lililobaki kwenye pochi lirudishwe, na kwenda namba gani ya pesa za simu au akaunti gani ya benki.
  • Tunaweza kukuomba uthibitishe ombi kwa kuingia kwenye akaunti, ili kuhakikisha hakuna mtu mwingine anayefunga akaunti yako.

Kisha tunafunga akaunti, tunatenganisha namba zako za WhatsApp na Mlango, na kufuta wasifu wako, wateja (contacts), makundi, violezo (templates), kampeni, ujumbe, mazungumzo ya Inbox na faili ulizopakia.

03Tunachotakiwa kubaki nacho

Baadhi ya kumbukumbu haziwezi kufutwa mara moja kwa sababu sheria inatutaka tuzihifadhi:

  • Kumbukumbu za fedha — kujaza salio, gharama na marejesho — kwa muda unaotakiwa na sheria za kodi na uhasibu za Tanzania (kwa kawaida miaka mitano). Hizi zinahifadhiwa kando na hazitumiki kwa jambo jingine lolote.
  • Kumbukumbu kwamba namba fulani ilijiondoa, ili isitumiwe ujumbe tena kwa makosa.
  • Taarifa zinazohitajika kutatua mgogoro au kutekeleza ombi halali la mamlaka, kwa muda wote mgogoro au ombi hilo linapoendelea.

Takwimu za ujumbe zinaweza kuhifadhiwa kwa namna isiyomtambulisha mtu yeyote.

04Inachukua muda gani

Tunakiri kupokea kila ombi ndani ya siku 7 na kulikamilisha ndani ya siku 30. Nakala zilizo kwenye hifadhi zetu za akiba (backups) zilizosimbwa hufutwa katika mzunguko wa kawaida wa akiba, ndani ya siku 30 zaidi.

Ujumbe ambao tayari umefika kwenye simu yako unabaki kwenye WhatsApp yako — uufute huko ukipenda. Meta huhifadhi kumbukumbu zake chini ya sera yake yenyewe.

05Maswali

Tuandikie kupitia habari@mlango.co.tz. Kama hujaridhika na jinsi tulivyoshughulikia ombi lako, unaweza kuwasilisha malalamiko kwa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Tanzania. Soma sera yetu kamili ya faragha.